ABOUT US

1. Introduction
M-TZ DIASPORA AWARDS & M-TZ TAIFA BOOK ni taasisi iliyosajiliwa kisheria kwa Kumb: Na. 549428 M-TZ pia kutambulika kupitia Mamlaka ya Hatimiliki Tanzania, COSOTA kwa Kumb: Na 2344L 1678440152 Sambamba na barua yenye Kumb Na.CST\DDEP\ORMIS\VOL.III\49.

M-TZ DIASPORA AWARDS
Tumejisaji kwa lengo la kuandaa tuzo za heshima kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi (DIASPORA AWARDS), kwa lengo la kutambua, kuthamini na kuheshimu mchango wao wa mambo makubwa mbalimbali wanayofanya kitaifa na kimataifa.

-Kuhamasisha diaspora kukumbuka nyumbani, kuwekeza nyumbani na kutoa fursa nyingi kwa Watanzania kupata koneksheni kimataifa.

-Tunaamini kupitia tuzo hizi zitaongeza kasi kubwa ya diaspora kuwekeza na kutoa fursa nyingi za Watanzania kwenda kufanya kazi nje.

1. M-TZ DIASPORA AWARDS NI NINI? Ni tuzo maalum za kutambua na kuheshimu michango ya baadhi ya Diaspora (Watanzania wanaoishi nje), ambao wamefanya mambo makubwa kitaifa na kimataifa kupitia nyanja za Elimu, Sanaa na Michezo, Afya, Utalii, Teknolojia, Habari na Mawasiliano, Kilimo, Ufugaji, Biashara, Network, Koneksheni, Ujasiriamali, Ubunifu NK.

2. M-TZ TAIFA BOOK NI NINI? Ni kitabu maalumu ambacho kinaandika matukio ya Watanzania wote kwa ujumla (DIASPORA NA WASIO DIASPORA) ambao wamefanya mambo makubwa kwenye Taifa kupitia Uongozi, Siasa, Uchumi, kijamii, Teknolojia, Ubunifu, Michezo, Biashara, Kilimo, Ufugaji, Elimu, Utalii, Afya NK.

M-Tz Taifa Book itasaidia vizazi vijavyo kuweza kujua historia ya taifa letu lakini pia kujua nani alichangia nini katika nchi.

Kutunza kumbukumbu muhimu za Watanzania waliothubutu , waliofanya mambo kadha wa kadha ambayo yameleta mabadiliko makubwa katika taifa kupitia Nyanja mbalimbali.

OUR MISSION:

-Kuandaa tuzo za heshima kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi (DIASPORA AWARDS).

Kutambua, kuthamini na kuheshimu mchango wao wa mambo makubwa mbalimbali wanayofanya kitaifa na kimataifa. Kuhamaisha diaspora kukumbuka nyumbani, kuwekeza nyumbani na kutoa fursa nyingi kwa Watanzania kimataifa.

-Kuhamasisha diaspora kuongeza kasi kubwa ya kuwekeza na kutoa fursa nyingi za Watanzania kwenda kusoma na kufanya kazi nje.

OUR VISSION

-Kutoa tuzo za heshima (Recognation Awards) na vyeti vya utambuzi (certificate of recognition) kwa wana diaspora mbalimbali ambao watastahili kutokana na mchango wao kwa taifa na kimataifa.

-Kukusanya taarifa za diaspora mbalimbali duniani waliofanya mambo makubwa ya kulijenga taifa letu.

-Kuthamini- michango mbalimbali inayotolewa na diaspora kwa ajili ya kulitangaza na kulijenga taifa letu.

-Kuhamasisha -diaspora kuendelea kufanya uwekezaji na ujenzi wa taifa letu kwa kasi zaidi. Kwani kila atakayepata tuzo atahamasika zaidi katika kuwekeza na kusaidia ukuaji wa nchi kiuchumi.

-Kuwajenga- Vijana wa kitanzania wengi kuwa na moyo wa kuthubutu, kujituma, uaminifu, kutengeneza fursa au koneksheni mbalimbali ndani na nje ya nchi.

-Kuheshimu- michango ya diaspora kwa taifa letu na Watanzania wasio diaspora ambao wamefanya makubwa katika maendeleo ya taifa letu.

-Kuelimisha-Watanzania na hasa vizazi vijavyo kuona umuhimu wa kuwekeza nyumbani hata kama utaenda nje ya nchi.

-kuongeza hamasa kwa Watanzania kuwa wabunifu na wazalendo wa kuijenga na kuipenda nchi yao.

-Kujenga na kudumisha mila na tamaduni za Kitanzania kwa Watanzania mbalimbali hata kama wanaishi nje ya Tanzania.

-Kuwakumbusha na kuhamasisha diaspora kuendelea kujitoa kwa ajili ya kujenge nchi yetu na kuwatia moyo vijana wapambanaji.

-Kujenga mahusiano bora ya moja kwa moja kwa diaspora wote kupitia M-Tz Diaspora Awards pamoja na kutambua fursa mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.



DIASPORA TEAM




Gabriel S. Ng'osha
CEO & Founder
Phone Number: +255 679 979 785
Whatsup NO: +255 679 979 785

Simon Gregory
Secretary General
Phone Number: Null
Whatsup NO: Null

Muhammad Sekamba
Coordinator
Phone Number: Null
Whatsup NO: Null

Elizabeth Mwabulanga
Treasurer
Phone Number: Null
Whatsup NO: Null

John Paul
Consulta/Connectors
Phone Number: Null
Whatsup NO: Null

Mohammed Chande
Organiser
Phone Number: Null
Whatsup NO: Null

Annastazia
Consulta/Connectors
Phone Number: Null
Whatsup NO: Null

Abdallah Kipunde
ICTO
Phone Number: +255 788377879
Whatsup NO: +255 788377879